Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela alishiriki katika mazishi ya Mama Mkwe wa Mkuu wa jimbo la Kaskazini Dayosisi ya Mashariki na Pwani(DSM) Mch Hunter Muro, Mama Emiliana Magava ambaye pia ni Mama Mdogo wa wabunge Mh.Venance Mwamoto na Mh.Rita Kabati.
Mazishi hayo yalifanyika wilaya ya Kilolo Iringa. Akiwafariji wafiwa Mh Kasesela alisema " Kuna aina mbili ya vifo hapa duniani vipo vifo kwa mapenzi ya Mungu kama Mama yetu Emiliana lakini pia vipo vifo vya kujitakia ambavyo tunamsingizia Mungu eti mapenzi yake" .
Aliendela kwa kuvitaja vifo kama kuendesha bodabdoa ovyo na kwa mbwembwe bila kuvaa kofia, kuendesha gari umelewa na vingine vingi vinavyo fanana.
Katika kutoa shukrani Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo ambaye pia alikuwa msemaji wa familia alisema imefika wakati wachungaji waruhusiwe kuchapa viboko kwani waumini wamekuwa na kiburi sana.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela ( kulia ) akiongea jambo na Mh.Venance Mwamoto wakati wa mazishi hayo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni