Mchezaji Ciaran Clark amejifunga na
kupelekea timu yake ya Jumhuri ya Ireland, kupata sare chungu katika
mchezo wao wa kwanza wa michuano ya Euro dhidi ya Sweden Jijini
Paris.
Wes Hoolahan aliipatia Ireland goli
la kuongoza mara tu baada ya mapumziko ya kipindi cha kwanza kwa
kuachia shuti kali zuri.
Hata hivyo presha ya Sweden ya
kutaka kurudisha goli hilo iliwazidi mabeki wa Ireland baada ya
Ciaran Clark kujikuta akijifunga akiunganisha krosi ya mpira wa chini
iliyopigwa na Zlatan Ibrahimovic.
Ciaran Clark akijifunga goli kufuatia krosi iliyopigwa na Ibrahimovic
Mpira uliopigwa na Wes Hoolahan ukiiandikia Jamhuri ya Ireland goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni