Wachezaji Emanuele Giaccherini na
Graziano Pelle wamefunga goli moja kila mmoja wakati Italia ikianza
kampeni yake ya kutwaa kombe la Euro 2016 kwa ushindi dhidi ya
Ubelgiji.
Mchezaji wa Sunderland, Giaccherini
aliifungia Itali goli la kwanza kufuatia pande safi alilopewa na
Leonardo Bonucci, huku mchezaji wa Southampton's Pelle akifunga goli
la pili.
Katika mchezo huo Ubelgiji
ilionekana ikiwa imechanganyikiwa huku Romelu Lukaku pamoja na Divock
Origi wakipoteza nafasi za kufunga.
Emanuele Giaccherini akipachika goli
Graziano Pelle akipiga shuti lililoandika goli la pili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni