Rais mteule wa Philippines, Rodrigo
Duterte, amewahamasisha wananchi wa nchi hiyo kuwapiga risasi na
kuwauwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya na kukabiliana nao katika
makazi yao.
Katika hotuba yake kwa njia ya
televisheni jana rais huyo amewasihi wananchi kusaidia vita dhidi ya
uhalifu, na ameahidi kuwapatia zawadi wale wote watakaoshiriki vita
hiyo.
Kauli hiyo ya rais Duterte
imeonekana kuungwa mkono na Meya moja ambaye ameipatia polisi zaidi ya paundi 2,000 kwa kuwauwa wasafirishaji dawa za kulevya.
Rais mteule wa Philippines Rodrigo
Duterte kati kati akipiga Selfie
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni