Maziko makubwa yatafanywa ya bondia
mkongwe bora duniani Muhammed Ali siku ya Ijumaa ili kuruhusu kila
mtu ambaye angependa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Ali,
familia yake imesema.
Maziko hayo ya Ali yatafanyika
kwenye mji wa nyumbani kwao wa Louisville, Kentucky, ambapo kwa
mujibu wa ratiba rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton amepangwa
kusoma wasifu wa Muhammed Ali.
Katika orodha ya wazungumzaji wakati
wa maziko ya Muhammed Ali, pia yupo Mchekeshaji Billy Crystal,
mwandishi wa habari za michezo Bryant Gumbel.
Bondia huyo mkongwe bingwa wa uzito
wa juu mara tatu alifariki dunia Ijumaa akiwa na umri wa miaka 74,
kwa kifo cha kawaida kilichosababishwa na ugonjwa ambao bado
haujabainishwa.
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton akiwa na Muhammed Ali
Rais Barack Obama akisalimiana na Muhammed Ali
Mtoto aliyefika kuomboleza kifo cha Muhammed Ali akiweka shada la maua
Muombolezaji akiwa amepiga goti kwa hisia kali katika eneo la kuweka mashada ya maua huko Louisville, Kentucky.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni