Klabu ya Manchester United ya
Uingereza imetenga dau la paundi milioni 30 ili kumnasa beki wa kati
wa timu ya Villarreal raia wa Ivory Coast, Eric Bailly, ambaye
anaaminika kuwa anakiwango cha juu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka
22, alikuwa anafuatiliwa kwa karibu na timu za Manchester City,
Bayern Munich na Arsenal katika siku za hivi karibuni lakini
Manchester United ndio wamekuwa wa kwanza kutoa dau.
Bailly aliyeachwa katika kikosi cha
Ivory Coast kilichoivaa Gabon hapo jana, pia timu za Barcelona na
Leicester zilikuwa zikimfuatilia tangu Januari lakini Villarreal
wanaimani kuwa anaweza akaenda Manchester United.
Beki Eric Bailly akiwa kibaruani dimbani
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni