Polisi nchini India wamesema
wamebaini biashara haramu ya figo za binadamu katika moja ya
hospitali ya binafsi kubwa katika Jiji la Delhi.
Polisi wa nchi hiyo wamesema watu
watano wamekamatwa hadi sasa, wakiwemo wafanyakazi wawili wa
hospitali ya Apollo.
Watuhumiwa hao wanahisiwa kuwa
wamekuwa wakiwashawishi watu masikini, kuuza figo zao kwa dola
zipatazo 7,500, na kisha wao kuziuza kwa bei ya juu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni