Timu
ya Liverpool ya Uingereza imeichakaza Barcelona kwa magoli 4-0 katika
mchezo wa kombe la Kimataifa la Mabigwa katika dimba la Wembley.
Katika
mchezo huo Sadio Mane alikuwa wakwanza kuifungia Liverpool goli
kufuatia shambulizi lililofanywa kwa kuwahusisha Adam Lallana na
Philippe Coutinho.
Mchezaji
wa zamani wa Liverpool Javier Mascherano alijifunga baada ya kipindi
cha pili na kuizawadia timu yake hiyo ya zamani goli la pili.
Divock
Origi aliongeza goli la tatu kwa Liverpool kwa kuupitisha mpira kati
kati ya miguu ya Claudio Bravo na baadaye Marko Grujic alifunga goli
la nne kwa kichwa cha kunyanyua.
Mchezaji mpya wa Liverpool Sadio Mane akiifungia timu hiyo goli la kwanza
Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi akishangilia goli lake alilofunga
Kipigo kikiwaacha hoi wachezaji wa Barcelona Luis Suarez na Lionel Messi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni