.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 7 Agosti 2016

PAUL POGBA NA RAPA DRAKE WATANUA PAMOJA KWENYE KLABU MAREKANI

Urafiki baina ya rapa Drake na Paul Pogba umeendelea kushika kasi baada ya wawili hao kupigwa picha wakiondoka kwenye klabu ya usiku Jijini New York Marekani jana majira ya alfajiri.

Rapa huyo Mmarekani na mchezaji mpira anayesakwa kwa fedha nyingi, wamekuwa wakila bata, huku Pogb akimkabidhi Drake jezi yake ya Juventus aliyoiweka saini yake baada ya kuhudhuria tamasha huko Madison Square Garden.

Wawili hao waliendelea kuikaribisha wikiendi wakiwa pamoja, huku mchezaji huyo anayewaniwa na Manchester United akiambatana tena na Drake katika kiwanja cha starehe cha Beautique Lounge Jijini New York. 
                        Pogba akimpatia Drake t-shirt yake ya Juventus yenye jina lake
                  Paul Pogba akitoka klabu baada ya kuponda starehe Jijini New York 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni