Mwanariadha
wa Afrika Kusini aliyefungwa Oscar Pistorius amepatiwa matibabu
hospitali, huku kukiwa na taarifa kuwa ameumia kwenye viwiko vyake vya viganja.
Msemaji
wa gereza amekataa kutoa taarifa za majeraha ya mwanariadha huyo
mlemavu, kwa madai kuwa ya usiri wa maradhi ya mgonjwa. Amesema
Pistorius alijiumiza baada ya kuanguka kitandani.
Mwezi
uliopita waendesha mashtaka walisema kifungo cha miaka sita
alichopewa kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp ni kidogo watakata
rufaa.
Reeva Steenkamp wakati wa uhai wake akiwa na Oscar Pistorius
Gereza alilofungwa mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni