Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akitambulisha viongozi waliompokea Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi
Makamu wa rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu na kijana wa CCM
Makamu wa rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akijaza kitabu cha majina ya wageni
Na. Emmanuel Amas
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufunga maonyesho hayo ya Nane nane hapo kesho kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli.
Alipowasili ikulu ndogo mjini Lindi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa LINDI Godfrey Zambi pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali na wa vyama vya siasa.
Katika Msafara wake, Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Kilimo, Maliasili na Uvuvi wa Zanzibar Mhe. Hamad Rashid.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni