Watu
wapatao 20 wamekufa kufuatia mvua ya gharika katika Jiji Kuu la
Skopje nchini Macedonia iliyosababisha mafuriko.
Miili
ya watu waliokufa imepatikana leo majira ya saa 8:30 asubuhi maafisa
wa nchi hiyo wamesema na kuongeza kuwa watu sita hawajulikani walipo.
Baadhi
ya waathirika walikufa maji wakiwa ndani ya magari yao. Mafuriko hayo
pia yamesomba lami katika baadhi ya barabara za Jiji hilo pamoja na
magari.
Watu wakikatiza kwenye maji yaliyotokana na mvua hiyo kubwa
Magari yaliyosombwa na maji ya mafuriko yakiwa yamepandiana
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni