Manchester United wamekamilisha
uhamisho uliovunja rekodi ya dunia wa paundi milioni 100 kwa kunasa
saini ya Paul Pogba.
Kiungo huyo mwenye kipaji
anayehitajika mno duniani anatokea Juventus, akijiunga tena na klabu
hiyo aliyoondoka kwa ada ya uhamisho sawa na bure mwaka 2012.
Pogba, 23, anatarajiwa kuvaa jezi
namba 6 na ametia saini mshahara wa paundi 290,000 kwa wiki katika
mkataba wa miaka mitano akinolewa na Jose Mourinho.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni