![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhpXmIAvOrE_goDl2aGfCxtkvblJMtMKA2RhE39T3TSShWZZWdKcu5V3a0LRjglaEVskUxtGtB4km9XyFSBHAO4FWh6YfVLzPjqq2ukRKAJiYGPMj5xy09tfw_2JFa_ME7dQ3oM8JbchnYh/s640/Ba.jpg)
Mabingwa watetezi wa ligi ya La Liga
Barcelonawamepata kipigo kutoka kwa timu iliyopanda daraja ya Alaves
wakati kocha Luis Enrique aliposhusha kikosi chake akiwaacha benchi nyota wake Lionel Messi na Luis Suarez.
Katika mchezo huo mshambuliaji
Mbrazili Deyverson aliwanyamazisha mashabiki wa Barcelona katika
dimba la Nou Camp alipounganisha wavuni mpira wa krosi kutoka kwa Kiko
Femenia kwa umbali wa yadi saba.
Beki Jeremy Mathieu aliisawazishia
Barcelona kufuatia kona iliyopigwa na Neymar aliyetokea benchi, hata
hivyo Ibai Gomez aliifungia Alaves goli la ushindi na kufanya matokeo
kuwa Alaves 2-1 Barcelona.
Deyverson akishangilia goli lake aliloitungua Barcelona
Beki Jeremy Mathieu akifunga kwa kichwa goli pekee la Barcelona
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni