Liverpool imewashinda kirahisi
mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza Leicester katika mchezo
wao wa kwanza wakichezea katika dimba la nyumbani katika msimu huu.
Wekundu hao walionekana hawakamatiki
baada ya Roberto Firmino kuunganisha pande la James Milner na
kuandika goli la kwanza, kicha Daniel Sturridge kutoa pasi ya
kisigino iliyofungwa na Sadio Mane.
Roberto Firmino akitoka nduki kushangilia goli lake alilofunga
Jamie Vardy akiokota mpira wavuni baada ya kufunga goli pekee la Leicester City
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni