Ilimchukua dakika sita tu Cristiano
Ronaldo kufunga goli lake la kwanza akirejea dimbani kwa mara ya
kwanza katika msimu huu na kuisaidia Real Madrid kuibuka na ushindi
mnono wa magoli 5-2 dhidi ya Osasuna.
Cristiano Ronaldo, aliyerejea
dimbani baada ya kuumia goti lake katika mchezo wa fainali ya Euro
2016 dhidi ya Ufaransa, aliunganisha wavuni mpira wa krosi uliopigwa
na Gareth Bale.
Danilo alifunga goli la pili. Sergio
Ramos na Pepe walifunga kwa kichwa mipira ya kona ya Toni Kroos na
Luka Modric kufunga la tano, kabla ya Oriol Riera na David Garcia
kuchomoa mawili.
Cristiano Ronaldo akiunganisha wavuni krosi ya Gareth Bale
Cristiano Ronaldo akimkimbilia Gareth Bale kumpongeza kwa kumpasia pande lililoza goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni