Chelsea sio tu imeshindwa kupata
pointi tatu baada ya kupambana kiume na Swansea na kutoka sare ya
magoli 2-2, bali pia mchezo huo umeamuacha na hofu kocha wao Antonio
Conte.
Hii ni baada ya kapteni wa klabu
hiyo John Terry, kujikuta akipata jeraha la kwenye enka katika dakika
za mwisho za mchezo huo wa Ligi Kuu ya Uingereza.
John Terry alikwatuliwa na
mshambuliaji matata Leroy Fer, aliyeifungia Swansea goli na
kumfanya beki huyo aruke juu na kuumia.
Kapteni wa Chelsea John Terry akigugumia maumivu baada ya kukwatuliwa
Kapteni John Terry akiwa na fimbo maalum za kumsaidia kutembe baada ya kuumia
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni