Mshambuliaji mpya wa Nice Mario
Balotelli ametupia magoli mawili katika mchezo wake wa kwanza katika
ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Marseille, na kusema ulikuwa umuzi
mbaya kwake kujiunga na Liverpool.
Mchezaji huyo raia wa Italia
alifunga magoli manne katika michezo 28, akiwa na Liverpool
akinunuliwa kwa kitita cha paundi milioni 16 kutoka AC Milan mwaka
2014.
Akicheza kwa mkopo Balotelli katika
ligi ya Serie A alifunga goli moja katika michezo 20 akiwa na Milan
katika msimu ulioisha, kabla ya kusajiliwa kama mchezaji huru na
Nice.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni