Dogo Marcus Rashford anatarajiwa
kupatiwa nafasi ya kuanza katika kikosi cha Manchester United siku ya
Alhamisi kwenye mchezo wa Ligi ya Uropa dhidi ya Feyenoord.
Rashford ambaye amekuwa akikalia
benchi mara nyingi chini ya kocha mpya Jose Mourinho, anaonekana
kuanza kumkubali baada ya kuonyesha makali katika mchezo na Hull City
pamoja na wa Manchester City.
Akimzungumzia mchezaji huyo, kocha
Jose Mourinho amesema kwake mchezo unaofuata ndio mkubwa na kusema
kuwa Rashford atakuwepo katika kikosi kitakachoivaa Feyenoord.
Marcus Rashford akishangilia goli alilofunga dhidi ya Hull City
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni