Kocha Pep Guardiola ameibuka mshindi
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya kocha rafiki yake wa
zamani Jose Mourinho baada ya Manchester City kupata ushindi wa
magoli 2-1 dhidi ya Manchester United, Old Trafford.
Katika mchezo huo Kevin de Bruyne
alifunga kiufundi goli la kwanza na Kelechi Iheanacho akafunga la
pili baada ya shuti la de Bruyne kugonga mwamba katika mchezo ambao
Manchester City iliutawala katika dakika zote 45 za kwanza.
United ilizinduka kabla ya kipindi
cha mapumziko baada ya kipa Claudio Bravo kujikuta katika harakati za
kuokoa mpira wa adhabu uliomkuta Zlatan Ibrahimovic ambaye
aliisawazishia goli moja Manchester United.
Kevin de Bruyne akimpoteza mahesabu kipa David De Gea
Zlatan Ibrahimovic akiangalia mpira alioupiga ukitinga wavuni
Kocha Joes Mourinho akipeana mkono na kocha Pep Guardiola baada ya mpira kumalizika
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni