Mamlaka za nchini Korea Kaskazini
zimesema kuwa wanasayansi wake wamefanikiwa kutengeneza dawa ambayo
inauwezo wa kuizuia na kuponya magonjwa kama Ukimwi, Ebola, Mers,
Sars na Saratani.
Shirika la Habari la Korea (KNCNA)
limesema wanasayansi hao wametengeneza dawa hiyo iitwayo Kumdang-2
kutokana na mmea wa ginseng uliopandwa kwa mbolea iliyochanganywa na
madini mbalimbali yakiwemo ya dhahabu na platinum.
Magonjwa kama ya Sars, Ebola na Mers
ambayo yanauhusiano na mfumo wa kinga yanaweza kuponywa kwa urahisi
na sindano ya dawa ya Kumdang-2 ambayo inasemekana inaongeza kinga
imara mno mwilini.
Boksi lenye vichupa vya dawa ya sindano ya Kumdang-2
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akifurahia ugunduzi huo na wanasayansi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni