Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye (MB) leo Jumamosi Septemba 10, anatarajiwa kutembelea Ofisi za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapa chini
KOZI YA MAKOCHA WANAWAKE YAFUNGWA
Kozi ya makocha wa Mpira wa Miguu imefungwa leo Septemba 9, 2016 saa 5.00 asubuhi kwenye Ukumbi wa Hosteli ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Katibu Mkuu, Mwesigwa Selestine ndiye aliyefunga kozi hiyo ambako pamoja na mambo mengine, alitoa shukrani za pekee kwa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) akisema: “Tunajivunia kwa upendeleo huu, bila shaka ni kwa sababu hata wanafunzi wanaofanya kozi hii, wanafanya vema.”
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapa chini
LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA SIKU TATU MFULULIZO
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo mitano ya Mzunguko wa Nne.
Miongoni mwa michezo hiyo, itakuwa ni ile ya upinzani wa jadi kati ya JKT Ruvu itakayokaribishwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Mwadui itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapa chini
KOCHA MOHAMMED MSOMALI AZIKWA
Kocha na mchezaji mahiri wa zamani wa Timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mohammed Msomali amezikwa leo Septemba 9, 2016 kwenye makaburi ya Kola yaliopo barabara ya zamani ya Dar es Salaam-Morogoro.
Mbali ya wajumbe mbalimbali wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) waliohudhuria mazishi hayo kwa upande wa TFF iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi katika maziko hayo ya Msomali aliyefikwa na umauti akiwa na umri wa miaka 74.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapa chini
KILIMANJARO QUEENS YAENDA UGANDA
Baada ya jana Septemba 8, 2016 kuilaza Burundi kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa, Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa ya wanawake wa Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Queens’, inatarajiwa kuondoka leo kwenda Jinja, Uganda kwenye michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) maarufu kama Kombe la CECAFA itafanyika kwa siku tisa kuanzia Septemba 11, 2016.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapa chini
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni