Polisi wa kaskazini magharibi mwa
India katika jimbo la Haryana wataanza kukagua biriani inayouzwa ili
kuhakikisha haina nyama ya ng'ombe.
Ukaguzi huo wa polisi utafanyika kwa
ushirikiano na maafisa mifugo katika wilaya ya Mewat, Mwenyekiti wa
Tume ya Huduma za Ng'ombe Bhani Ram Mangla amesema.
Jamii ya Wahindu waliowengi
humchukulia mnyama ng'ombe kama mnyama mtakatifu lakini wahindi wengi
hula nyama. Ulaji nyama katika jimbo la Haryana umepigwa marufuku.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni