Serena Williams amepoteza nafasi ya
kwanza duniani aliyokuwa akiishikilia katika mchezo wa tenesi
wanawake, baada ya kushindwa katika hali ya kushangaza mchezo wa nusu
fainali za US Open dhidi ya raia wa Czech Karolina Pliskova.
Serena aliyekuwa anashikilia nafasi
hiyo ya tangu Februari 18, 2013, ameweza kuishikilia nafasi hiyo ya
juu katika mchezo huo kwa wiki 186 mfululizo, ambayo ni sawa na
rekodi iliyowekwa na Mjerumani, Steffi Graf.
Williams aliyepaswa kutinga fainali
ili aweze kujipa nafasi ya kuweza kuvunja rekodi ya Graf, alijikuta
akibugi mahesabu na kufungwa na mchezaji namba 10 Pliskova kwa seti
6-2, 7-6 (3) mbele ya umati wa watu Jijini New York katika mchezo
uliochezwa kwa saa mbili na dakika 26.
Karolina Pliskova akishangilia baada ya kushinda
Serena Williams akiinamisha kichwa chini baada ya kushindwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni