Makumi ya watalii wamekwama juu ya
magari ya kutumia waya katika Mlima wa Alps nchini Ufaransa na
kulazimu 45 kulala kwenye magari hayo usiku kucha, baada ya upepo
mkali kusababisha hitilafu ya kiufundi.
Zoezi la uokoaji lilifanywa kwa
watalii hao zaidi ya 110 kwenye magari hayo ya kukatiza juu ya mlima
kwa kutumia kamba wakiwa juu umbali wa mita 50 katika eneo la Mont
Blanc katika Mlima wa Alps.
Waokoaji wa mataifa ya Ufaransa,
Italia na Uswizi jana usiku walitumia helkopta kuokoa watalii 65 kati
ya 110 waliokuwa wamekwama, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Chamonix,
Bernard Cazeneuve amesema.
Waokoaji wakiwa wanafanya kazi ya uokoaji kwa kutumia helkopta
Baadhi ya watalii waliookolewa wakiwa na furaha
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni