Watu wa kabila la Torajan nchini
Indonesia wamekuwa wakijivunia kuwaonyesha ndugu zao waliofariki kwa
kuwafukua makaburini kila mwaka na kuwavalisha nguo mpya ikiwa ni
tambiko la kuonyesha heshima kwa waliokufa.
Kila mwaka kabila hilo lililopo
kisiwa cha Sulawesi huwafukua watu waliokufa, ambapo huwaosha na
kuwavalisha nguo mpya na kisha kujikusanya familia nzima na kupiga
picha na maiti ikiwa ni tambiko lijulikanalo kama Ma'nene.
Wazazi waliokufa wakiandaliwa baada ya kufukuliwa kwa ajili ya tambiko la Ma'nene
Wanafamilia wakipiga picha na ndugu yao maiti baada ya kumfukua, kumsafisha na kumvalisha nguo mpya
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni