Raia wa Scotland Andy Murray
amebakiza ushindi mmoja tu kuweza kuwa mchezaji tenesi namba moja
duniani, kufuatia Novak Djokovic kujikuta akishindwa na Marin Cilic
kwenye michuano ya Paris Masters.
Djokovic aliyekuwa akihitaji kutinga
fainali za michuano hiyo ili kuendelea kuitetea nafasi yake hiyo ya
mchezaji bora namba moja dunani alijikuta akipoteza bila ya kutarajia
kwa seti 6-4 7-6 (7-2) dhidi ya Cilic katika mchezo wa robo fainali.
Mchezaji namba mbili dunia kwa
mchezo huo Murray yeye alimfunga Czech Tomas Berdych kwa seti 7-6
(11-9) 7-5 na sasa atacheza na ria wa Canada Milos Raonic katika nusu
fainali itakayochezwa leo. Iwapo atashinda Murray atakuwa namba moja
kwa mara ya kwanza.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni