JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail:
press@ikulu.go.tz
Tovuti :
www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kesho
tarehe 04 Novemba, 2016 atafanya mahojiano ya kwanza na waandishi wa
habari tangu aingie madarakani mwaka mmoja uliopita.
Mahojiano
haya yatarushwa moja kwa moja na vituo vya habari vya redio na
televisheni kutoka ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam na yataanza
saa 4:00 asubuhi.
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais inapenda kuwaalika wananchi wote kusikiliza na
kutazama mahojiano hayo ili mpate fursa ya kujua mambo mbalimbali
ambayo Mheshimiwa Rais atayatolea majibu.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar
es Salaam
03
Novemba, 2016
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni