Timu ya Fenerbahce imefunga mara
mbili magoli mazuri dhidi ya Manchester United na kukifanya kikosi
hicho cha Jose Mourinho kuwa hatarini kuondolewa katika Ligi ya
Uropa.
Mshambuliaji Moussa Sow aliipatia
Fenerbahce goli la kuongoza katika sekunde ya 65 kwa kufunga kwa tik
taka na kisha Jeremain Lens kufunga goli la pili la mpira wa adhabu.
Katika mchezo huo Manchester United
ilishuhudia Paul Pogba alitoka nje baada ya kuumia, hata hivyo
baadaye Wayne Rooney alifunga goli pekee kwa timu yake kwa shuti la
yadi 25.
Moussa Sow akifunga goli la kwanza katika mchezo huo kwa tik taka
Jeremain Lens akishangilia goli lake alilofunga kwa kukimbia
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni