Mwenyekiti wa Jukwaa la Habari Tanzania (TEF), Theothil Makunga (kulia), akiwa na wajumbe wa jukwaa hilo, Jane Mihanji (katikati) baada ya kutoka bungeni Dodoma jana, kusikiliza mwenendo wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari.
Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge akiongoza majadiliano hayo
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani (kulia) akiwa na wapiga kura wake waliotembelea Bunge jana.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwasilisha bungeni Dodoma, Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akipongezana na naibu wake, Anastazia Wambura baada ya kuwasilisha muswada huo
Mbunge wa Tunduma, Mwakajoka akisalimiana na Mbunge wa Busanda, Leonecia Butimbaa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akijadiliana jambo na Mjumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEA), Jane Mihanji (kulia) na Saedy Kubenea kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma, baada ya kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari.
Waziri Kivuli wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Joseph Mbilinyi akiwasilisha bungeni, Dodoma jana, maoni ya Kambi rasmi ya Upinzani kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akichangia hoja bungeni Dodoma, kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016, ambapo alisema kuwa muswada huo hauwatendei haki wanahabari.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saedy Kubenea akichangia muswada huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni