Matumaini ya kusonga mbele katika
Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwa timu ya Tottenham, sasa yapo hatarini
baada ya kupata kipigo kingine wakiwa nyumbani dhidi ya Bayer
Leverkusen katika dimba la Wembley.
Katika mchezo huo Leverkusen ilipata
goli pekee mnamo dakika ya 65, na kuifanya Spurs ikijikuta ikitota
kwa mara ya pili katika michuano hiyo ikiwa katika uwanja huo wake wa
muda inaoutumia kwa sasa kutokana na uwanja wake wa White Hart Lane
kuwa kwenye matengenezo.
Kevin Kampl akifunga goli pekee katika mchezo huo
Nayo timu ya Leicester City
inachungulia kuingia katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
baada ya jana kufanikiwa kutoa sare tasa na FC Copenhagen.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni