Real Madrid itabidi wagojee kuweza
kujihakikishia kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya,
baada ya kutoka sare ya magoli 3-3 na Legia Warsaw, katika mchezo
uliochezwa bila mashabiki.
Mchezo huo ulichezwa bila
kuhudhuriwa na mashabiki kutokana na kutokea ghasia za mashabiki
katika mchezo uliopita wakati Legia ilipolala 6-0 dhidi ya Borussia
Dortmund na kutozwa faini ya paundi 69,000.
Katika mchezo huo Gareth Bale
aliweka rekodi ya kufunga goli la mapema kabisa kwenye ligi hiyo,
alilolifunga katika sekunde ya 57 tu ya mchezo na kisha baadaye
kumsaidia Karim Benzema kuongeza la pili.
Legia Warsaw ilizawazisha kupitia
kwa Vadis Odjidja-Ofoe na Miroslav Radovic na kisha kuongeza goli la
tatu lililofungwa na Thibault Moulin strike, hata hivyo Real Madrid
ilisawazisha dakika mbili baadaye kupitia kwa Mateo Kovacic.
Kipa wa Legia Warsaw akiruka bila ya mafanikio kuzuia mpira uliopigwa na Gareth Bale
Vadis Odjidia akifunga goli la jitihada binafsi na kufufua matumaini ya Legia Warsaw
Vadis Odjidia akifunga goli la jitihada binafsi na kufufua matumaini ya Legia Warsaw
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni