Mshambulia wa Real Madrid Cristiano
Ronaldo amemshinda mpinzani wake mkuu Lionel Messi na kushinda tuzo
ya mchezaji bora wa soka duniani 'Ballon d'Or'.
Ronaldo ameitwaa tuzo hiyo kwa mara
ya nne, huku mpinzani wake Messi akiwa ameitwaa tuzo hiyo kwa mara
tano ikiwemo mwaka jana.
Messi alishika nafasi ya pili katika
tuzo hizo na mshambuliaji wa Atletico Madrid Mfaransa Antoine
Griezmann akiwa katika nafasi ya tatu.
Ronaldo aliisaidia Real Madrid
kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya, na aliisaidia Ureno kushinda
michuano ya Euro 2016.
Ronaldo akiwa na Mama yake Maria na mwanae Cristiano Junior
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni