MKUU wa Maendeleo ya Soka la Vijana Azam FC, Tom Legg, jana Jumatatu ameanza kazi jana ya kuwafanyia mchujo vijana wenye umri chini ya miaka 15 na 17 waliochaguliwa kwenye majaribio ya wazi ya mkoa wa Dar es Salaam katika mpango wa Kitaifa wa timu hiyo wa kutengeneza timu za vijana wa umri huo.
Ni vijana 34 tu waliohudhuria kati ya 46, kwenye siku hiyo ya kwanza, ambapo vijana hao waliweza kupimwa uzito na urefu kabla ya kuingia uwanjani kufanya mazoezi mepesi na kucheza mechi ndogo ndogo baina ya wao wenyewe.
Zoezi hilo litaendelea tena kesho Jumatano, ambapo Legg anatarajia kumalizia programu hiyo Alhamisi ijayo kwa kuwachuja vijana hao na kubakia na wale bora. Vijana watakaochaguliwa kwenye orodha ya mwisho ya mkoa wa Dar es Salaam, wanatarajia kuungana na vijana wengine waliochaguliwa kwenye mikoa mbalimbali katika zoezi hilo katika mchujo wa mwisho unaotarajia kufanyika hivi karibuni mwezi huu ndani ya Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni