.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 17 Januari 2017

BALOZI SEIF AFANYA ZIARA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimjuilia Hali aliyekuwa Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Tanzania Bwana Makame Launi aliyelazwa Wadi ya Mapinduzi Kongwe katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja akipatiwa matibabu. Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameuagiza Uongozi wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kuharakisha matengenezo ya Mashine ya uchunguzi wa Maradhi ya Matumbo { Utra sound } ili kupunguza msongamano wa Wagonjwa wanaohitaji huduma hizo.

Alisema Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ndio kimbilio pekee la Wananchi wote wa Zanzibar wanalolitegemea kukidhi mahitaji yao ya dharura wakati wanapokumbwa na matatizo mbali mbali ya kiafya.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo wakati alipofanya ziara fupi ya kukagua chumba cha uchunguzi wa maradhi ya Matumbo katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ambapo Mashine moja kati ya Mbili zilizomo ndani ya chumba hico imeharibika kwa zaidi ya miezi miwili sasa.

Alisema mabadiliko ya kimaisha katika mazingira ya matumizi yasiyo sahihi ya vyakula mchanganyiko wanavyotumiwa Wanaadamu yamechangia ongezeko la mardhi tofauti yakiwemo yale yanayowasumbua akina Mama ya Matumbo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Ali Salum Ali alisema juhudi za matengenezo za Mashine hiyo tayari zimeshachukuliwa na Uongozi huo ili kuurejesha mpangilio wa huduma hizo uwe wa kawaida.

Hata hivyo Dr. Ali alisema kilichochelewesha kukamilika kwa matengenezo hayo ni mtaalamu wa kuifanyia marekebisho Mashine hiyo ambaye analazimika kutoka nje ya Zanzibar.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
17/1/2017.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni