Timu ya taifa ya DR Congo imeweka
kando hali ngumu ya kambi yake katika michuano ya mataifa ya Afrika
na kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Morocco katika mchezo wa
kundi C huku ikimaliza na wachezaji 10 tu.
Kikosi hicho kinachonolewa na
Florent Ibenge, ambacho kiligoma Ijumaa kutokana na kutolipwa posho
zao, walianza kwa kusuasua katika mchezo huo kwenye dimba la Stade
d'Oyem baada ya Mbark Boussoufa kupiga shuti lililogonga mwamba.
Alikuwa Junior Kabananga
aliyewafanya vijana hao wa Joseph Kabila kuongoza kabla ya mchezaji
aliyetokea benchi Lomalisa Mutambala kupewa kadi za njano mara mbili
ndani ya dakika 16 na kutolewa nje.
Katika mchezo mwingine jana mabingwa
watetezi wa Kombe la Mataifa ya Afrika Ivory Coast walijikuta
wakiambulia sare ya 0-0 dhidi ya Togo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni