Mbunge mmoja nchini Kenya amewataka
wanawake walipo kwenye maeneo ambayo ni ngome kuu ya upinzani nchini
humo kuwanyima unyumba wanaume wao ambao bado hawataenda
kujiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu.
Mbunge huyo mwakilishi wa wanawake
Mombasa, Bi. Mishi Mboko, amewaomba wanawake wenzake kuwanyima haki
yao ya ndoa wanaume wao ili kuwalazimisha kwenda kujiandikisha kupiga
kura katika uchaguzi wa Agosti 8.
Akiongea kwenye viwanja vya Jomo
Kenyatta huko Mkomani, Mombasa ambako alitoa hundi kwa kikundi cha
vijana, Bi. Mishi amesema kuwanyima unyumba wasiojiandikisha
kutawafanya wanaume waharakishe kujiandikisha kupiga kura katika
zoezi lililoanza jana.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni