Wakala wa Diego Costa, Jorge Mendes,
alisafiri kwenda China kufanya mazungumzo na mmiliki wa timu yenye
kisu kirefu cha usajili ya Tianjin Quanjian, Shu Yuhui.
Mshambuliaji huyo wa Chelsea
amekwaruzana na kocha wake Antonio Conte kuhusina na kutokuwa fiki
huku kukiibuka taarifa za kupewa ofa nono kutoka Ligi Kuu ya China.
Mmiliki wa klabu ya Tianjin
Quanjian, Shu Yuhui amesema kuwa amefanya mazungumzo na wakala Mendes
na kudai kuwa Costa ataruhusiwa kuondoka Chelsea mwishoni mwa msimu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni