Jumamosi, 14 Januari 2017
BALOZI SEIF ATEMBELEA MAONYESHO YA TAMASHA LA TATU LA BIASHARA VIWANJA VYA MAISARA
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akibadilishana mawazo na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum katika chumba cha VIP kwenye Viwanja vya Maisara kabla ya kutembelea Mabanda ya Maonyesho ya Tamasha la Tatu la Biashara kuadhimisha sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Miaka 53.
Afisa wa kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Nd. Makame Haji Mohamed akimueleza Balozi Seif kazi za Idara hiyo wakati alipotembelea maonyesho ya Tamasha la Biashara Zanzibar.
Balozi Seif akifurahia ubunifu wa kazi za wajasiri amali wa Zanzibar katika mbinu za kusarifu udongo na hatimae kuwa bidhaa zilizoingia kwenye soko linalokubalika na jamii.
Wajasiri amali kutoka Mkoa wa Kilimanjaro Tanzania Bara walioshiriki Maonyesho ya Tamasha la Tatu la Biashara Zanzibar Hapo Maisara Suleiman wakimpatia maelezo Balozi Seif jinsi ya mali ghafi ya ngozi wanavyoweza kutengeneza bidhaa za mikoba na Viatu.
Balozi Seif akiridhika na taaluma kubwa iliyotumiwa na wajasiri amali wa Taasisi ya Waasili Asilia { WA } katika kutengeneza bidhaa zinazotokana na rasilmali ya ngozi. Picha na – OMPR – ZNZ.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni