Timu ya Guinea Bissau imewashangaza
wengi baada ya kutoa sare ya goli 1-1 na Gabon wenyeji wa Michuano ya
Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon), hii ikiwa ni mara ya kwanza
kucheza michuano hiyo.
Goli la kusawazisha la Guine Bissau
ambayo ni moja ya mataifa masikini ya Afrika lilifungwa na Soares kwa
kichwa cha kuchupa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa katika
dakika ya 90.
Gabon walipata goli lao la kwanza
katika dakika ya 52, kupitia mshambuliaji wao nyota anayechezea
Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang akitumbukiza kimiana
krosi ya Denis Bouanga.
Pierre-Emerick Aubameyang akiwa haamini kilichotokea
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni