Timu ya Burkina Faso imepambana
kiume na kufanikiwa kutoa sare ya goli 1-1 na Cameroon katika siku ya
kwanza ya ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).
Cameroon ilipata goli la kuongoza
katika dakika ya 35, kupitia kwa mpira wa adhabu uliopigwa kiufundi
na Benjamin Moukandjo na kujaa kwenye kona ya juu ya goli.
Timu zote mbili zilitengeneza nafasi
nzuri, ambapo moja ya nafasi ya wazi ilimkuta Clinton N'Jie ambaye
alipiga shuti lililoenda njea ya goli.
Benjamin Moukandjo akipiga kiufundi mpira wa adhabu na kufunga goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni