Ndege ya jeshi la Nigeria
imedondosha kimakosa bomu kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani
Kaskazini-Mashariki mwa nchi hiyo na kuuwa watu 52 pamoja na kujeruhi
wengine kadhaa.
Watumishi wa misaada ni miongoni mwa
watu waliokufa katika kambi ya Rann, ambapo Chama cha Msalaba
Mwekundu kimesema wafanyakazi wake sita wameuwawa katika tukio hilo.
Shirika la misaada la Madkatari
Wasio na Mipaka (MSF) limesema zaidi ya watu 200, wamejeruhiwa
wameomba msaada wa usafri wa majeruhi kutoka kambi hiyo.
Rais Muhammadu Buhari, ambaye jeshi
lake linapigana na kundi la Boko Haram ameonyesha kusikitishwa na
tukio hilo na kuomba utulivu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni