.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 13 Januari 2017

HALMASHAURI YAIFUNGIA KWA MUDA USIOJULIKANA SHULE YA MSINGI HAZINA MISION KWA KUTOKUWA NA VIWANGO VYA UANDIKISHAJI

Na Woinde Shizza,Arusha

HALMASHAURI ya jiji la Arusha imeifungia kwa muda usiojulikana shule ya msingi Hazina Mision iliyopo kata ya Baraa mara baada ya uongozi wa shule hiyo kushutumiwa kwa makosa mbali mbali ikiwemo kuwatelekeza watumishi
wake pamoja na mindombinu kuwa chini ya viwango vinavyohitajika katika uandikishaji wa shule.


Hatua hiyo ya kufungiwa kwa shule hiyo imekuja mara baada siku chache
zilizopita wamiliki wa shule hiyo kulalamikiwa kuwanyanyasa na kushindwa
kuwalipa mishahara watumishi na walimu wa shule hiyo na hivyo kutakiwa
kufanya marekebisho na kuwalipa stahiki watumishi lakini wakakaidi kufanya
maagizo hayo kwa muda waliopewa.

Akitoa agizo hilo katika viwanja vya shule hiyo kaimu afisa elimu shule za
msingi katika jiji la arusha Eunice Elibariki alisema kuwa wameamua
kusimamisha huduma ya utoaji elimu kutokana na shule hiyo kushindwa kufanya marekebisho waliyotakiwa kuyafanya shuleni hapo.

Alisema kuwa awali kabla hatua hiyo haijafikiwa walipata taarifa kuwa
uongozi wa shule hiyo inawanyanyasa walimu kwa kuwanyima mishahara yao,
kutokuwa na mindombinu kuachilia viwango pamoja na kuwepo uchafuzi wa
mazingira na ndipo uongozi ukapewa muda wa kufanya marekebisho hayo pamoja na kimaliza migogoro ya kimaslahi lakini walikaidi kutoa ushirikiano hali iliyopelekea halmashauri hiyo kuchukua hatua ya kusimamisha utoaji huduma.

"Kwa kuwa uongozi wa shule hii mlishindwa kufanya marekebisho mlioagizwa
ikiwa ni pamoja na kishindwa kumaliza migogoro ya walimu kuanzia sasa
nasimamisha huduma za masomo hadi hapo mtakapoweza kuiweka shule yenu katika mazingira yanayohitajika kwani lazima shule iwe na viwango na sifa zinavyohitajika sio tu kuendesha kiholela "alisema Eunice

Wananchi wa eneo hilo akiwemo Diwani wa kata ya baraa Elifasi Ndetika
akizungumzia uamuzi wa kufungiwa kwa shule hiyo alisema kuwa ni halali
kabisa kwani walikuwa na malundano ya muda mrefu baina ya uongozi na walimu lakini walishindwa kumaliza wenyewe huku akidai kuwa mazingira yalikuwa hayadhirishi na hivyo kupitia usimamishaji huo unaweza kupelekea
marekebisho yakawepo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni