.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 28 Januari 2017

MABONDIA MBWANA MATUMLA NA MESHACK MWANKEMWA WATAMBA KUWADUNDA WAPINZANI WAO FEB 5 TAIFA


Bondia Mbwana Matumla kushoto akielekezwa kupiga ngumi na Said Abdulghafoor wakatio wa mazoezi ya Matumla ya kutambulisha mpambano wake na Seleiman Shabani utakaofanyika Feb 5 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Mesharck Mwankemwa wa Mbeya na Mbwana Matumla wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mazoezi yao ya kujiandaa na mapambano yao yatakayofanyika Feb 5 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Mwankemwa atapanda ulingoni na Ramadhani Shauri na Matumla atamkabili Seleiman Shabani Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Mesharck Mwankemwa wa Mbeya na Mbwana Matumla wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mazoezi yao ya kujiandaa na mapambano yao yatakayofanyika Feb 5 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Mwankemwa atapanda ulingoni na Ramadhani Shauri na Matumla atamkabili Seleiman Shabani Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Mbwana Matumla kushoto akipambana na Meshack Mwankemwa wakati wa mazoezi yao ya mwisho mwisho kabla ya mpambano wao na wapinzani wao Feb 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa Matumla atapambana na Seleiman Shabani na Mwankemwa atakabiliana na Ramadhani Shauri Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa Mchezo wa Masumbwi nchini Shomali Kimbau akimwelekeza bondia Meshack Mwankemwa wakati wa mazoezi yake kwa ajili ya kujiandaa na Ramadhani Shauri Feb 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS


Wadau wa mchezo wa masumbwi nchini wakimfuraia Bondia Mbwana Matumla wa tatu kushoto akipeana mkono na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wengine kutoka kushoto ni William Kaijage Said Abdulghafoor Juma Mbili pamoja na Chaurembo Palasa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Mbwana Matumla anataraji kupanda ulingoni tena baada ya kukaa mnje ya ulingo tangia mpambano wake wa mwisho aliocheza katikas ukumbi wa Dar Live Desemba 25 mwaka 2012 alivyo msambalatisha bondia David Chalanga Nairobi, Kenya anarudi tena ulingoni Feb 5 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa kupambana na Suleimani Shabani mpambano wa raundi nane uzito wa Super Feather Weight


Mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka likiwemo la bondia Meshack Mwankemwa atakaepambana na Ramadhani Shauri, wakati Mohamed Matumla atavaana na Mfaume Mfaume

na Twalibu Tuwa wa Kiwangwa Bagamoyo atavaana na Saidi Chino mpambano wa ubingwa wa Taifa raundi kumi na Husein Pendeza wa Ashanti Boxing clab ya Ilala atakaevaana na Said Hamdani kutoka Mbezi Conetion


Mkwela atazipiga na Manyi Issa mpambano wa raundi kumi kumasliza ubishi wa nani zaidi ya mabondia hao ambapo Mkwela anafundishwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' na Issa anaefundishwa na Amos Martin Nkondo kutoka Mbezi Conetion


Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni