.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 28 Januari 2017

PASS YAWATAKA WAKULIMA,WAFUGAJI NA WAVUVI KUFANYA SHUGHULI ZAO KITAALAM


Nicomed Bohai ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kusaidia Sekta Binafsiya Kilimo Taifa (PASS)Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya wakulima wakipata maelekezo katika Pass katika maonyesho ya zana za kilimo yaliyofanyika Jijini Arusha na kumalizaika jana maonesho hayo yalikuwa ya siku mbili.Picha na Vero Ignatus Blog.

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Asasi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo (Pass)imewataka wakulima na wajasiriamali wote wa kilimo ,uvuvi na wafugaji wafikirie namna ya shughuli zao kitaalam.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa asasi hiyo Nicomed Bohai ya kwamba wakulima wafikirie kufanya shughuli zao kibiashara,watafute elimu na maarifa ili waweze kudhaminiwa kupata mkopo wa kuendeleza shughuli zao.

Amesema kuwa wanajenga mahusiano ya kibiashara kutoka kwa wafanya biashara wakubwa kwenda kwa wadogo,ili wale ambao wameshapiga hatua wawainue wale ambao bado,kwa kutengeneza mchanganuo wa kibiashara na kutoa udhamini wa mkopo.

Aidha mkurufenzi huyo amesema kuwa Asasi hiyo ya kusaidia sekta binafsi ya
kilimo ipo tayari kumsaidia mtu binafsi,vikundi au makampuni kutumia huduma ya (Pass)haswa wajasiariamali binafsi amabao wana dira ambao wanafanya biashara katika hali ya ufanisi na kibiashara.

Sambamba na hayo amesema ya kwamba asasi hiyo inashirikiana na benki washirika zaidi ya 11 kupata mkopo kwa wakulima ambao wanaoweza kufikia angalau vigezo vya msingi kwaajili ya ukopaji,huku kipaumbele kikitolewa kwa wateja wenye matokeo makubwa katika mwendelezo wa mnyororo wa thamani kwa bidhaa za kilimo hususani katika mazao ya chakula ,biashara na mazao ya kusafirishwa nje ya nchi.

Ameainisha mikoa ambayo Pass ipo nchini Tanzania kuwa ni Mwanza ,Kigoma,Kilimanjaro,Morogoro,Mbeya, Dar-es- salaam na Mtwara,amesema wanatumia ofisi hizi za kanda ili kuwafikia wakulima kwa karibu zaidi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni