.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 29 Januari 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA KATIKA KUTANGAZA JINA RASMI LA KITUO CHA AMANI NA USALAMA KILICHOPEWA JINA LA MWALIMU JULIUS NYERERE KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRICA (AU) ADDIS ABABA NCHINI ETHIOPIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Viongozi Wakuu wa Mataifa mbalimbali hawapo (pichani) katika Jengo jipya la Kituo cha Amani na Usalama kilichopewa jina Rasmi la Mwalimu Julius Nyerere, Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kutangazwa rasmi kwa Jina la Mwalimu Julius Nyerere katika kituo hicho cha Amani na Usalama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakielekea katika Kituo cha Amani na Usalama cha Makao Makuu ya Umoja wa Afrika kilichopewa jina la Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, Addis Abba nchini Ethiopia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na viongozi wa mataifa mabalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika jengo jipya la kituo cha Amani na Usalama (JULIUS NYERERE) lililopo katika Makao makuu ya Umoja wa Afrika Addis Ababa nchini Ethiopia. PICHA NA IKULU

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni