Wachimbaji 15 waliokuwa wamefukiwa
na kifusi katika mgodi wa dhahabu wa RZ uliopo Nyarugusu, Mkoani
Geita nchini Tanzania wameokolewa wote leo asubuhi wakiwa hai.
Wachimbaji hao walifukiwa na kifusi
tangu siku ya Alhamis wamefanikiwa kuokolewa kufutia jitihada
zilizofanywa na waokoaji bila kukata tamaa na hatimae kuzaa matunda
leo.
Hapo jana vikosi vya uokoaji
vilifanikiwa kushusha chini aridhini tochi na radio kwa kutumia drill
na kamba ikarudi tupu wakajua vitu hivyo vimepokelewa.
Wakashusha barua, kalamu na karatasi
na vipapokelewa na kujibiwa kwa maandishi kuwa wachimbaji hao wapo 15
na mmoja wao ameumia kwa kuchomwa na msumari.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni