Real Madrid wamepoteza michezo
miwili mfululizo tangu Novemba 2015 kwa kufungwa magoli 2-1 na Celta
Vigo katika mchezo wa awali wa kombe la Copa del Rey.
Madrid, ambayo rekodi yake ya
kutofungwa michezo 40 mfululizo ilimalizwa na Sevilla jumapili,
walijikuta wakifungwa goli la kwanza na mchezaji wa zamani wa
Liverpool, Iago Aspas.
Wenyeji Real Madrid walisawazisha
kupitia kwa Marcelo kwa shuti kali la mguu wa kushoto, lakini Jonny
akaiongezea Celta Vigo goli la pili.
Iago Aspas akiwa ameachia shuti lililoandika goli la kwanza
Cristiano Ronaldo akitoka uwanjani akiwa na mawazo tele bada ya kipigo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni