Serena Williams amemfunga dada yake
Venus kwa seti mbili mfululizo na kushinda taji lake la saba la
Mashindano ya Tenesi ya Wazi ya Australia, na kuweka rekodi ya Grand
Slam ya 23.
Serena, 35, amemshinda Venus, 36,
kwa seti 6-4 6-4 na kumshinda Steffi Graf aliyekuwa akiongoza kwa
kushinda mara nyingi mashindano makubwa ya wachezaji wa kulipwa mwaka
1968.
Kwa ushindi huo Mmarekani huyo
aliyekuwa anashikilia namba mbili kwa ubora duniani katika uchezaji
tenesi, sasa amekuwa namba moja dunia akimpiku Mjerumani Angelique
Kerber.
Serena Williams akinyanyua kombe alilochukuwa huku dada yake Venus akiangalia
Wanadada ndugu Serena na Venus Williams wakikumbatiana baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa fainali
Serena Williams akiwa amekaa chini akishangilia kwa furaha baada ya kushinda
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni