Kampuni ya Google imewaita
wafanyakazi wake waliosafarini kurejea Marekani, badaa rais Donald
Trump kutoa amri ya kuzuia raia wa mataifa saba ya Kiislam kuingia
Marekani.
Katika agizo hilo wakimbizi kutoka
Syria wamezuiwa kuingia Marekani hadi hapo itakapotolewa agizo
jingine.
Raia wa mataifa sita ya kigeni
yakiwemo ya Iran na Irak watazuiliwa kuingia Marekani kwa muda wa
siku 90.
Pia programu yote ya kuandikisha
wakimbizi imesitishwa kwa siku 120 na kiwango cha chini cha kuchukua
wakimbizi kimeshushwa.
Jumamosi abiria kadhaa wa Irak na
Yemeni walizuiliwa kuingia kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa
Cairo kuelekea Jijini New York, licha ya kuwa na visa za Marekani.
Waandamanaji wakipinga sera za kuwabagua wahamiaji za rais Donald Trump
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni